JE TUTAKIMBILIA WAPI..? MAAFISA WEZI
Huduma ya taifa ya polisi NPS imekanusha madai kwamba maafisa wa polisi waliiba vipatakalishi kutoka madukani jijini Nairobi wakati wa maandamano ya kulalamikia mauaji ya mwalimu na mwanablogu Albert Ojwang.
Katika taarifa, NPS imeelezea kwamba inafahamu kuhusu video inayosambaa mitandaoni inayoonyesha afisa mmoja wa polisi akiwa amebeba vipatakalishi hivyo.
Mkurugenzi wa mawasiliano katika NPS Muchiri Nyaga aliendelea kusema kwamba polisi hao walikamata mshukiwa mmoja na kumpokonya vifaa hivyo vya kielektroniki, ambavyo vimehifadhiwa katika kituo cha polisi cha Central Nairobi kama idhibati.
Huduma hiyo ya taifa ya polisi imesema inaendeleza uchunguzi kwa lengo la kukamata waliohusika na visa vya uhalifu wakati wa maandamano ya jana, ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Copied from known sources
Comments
Post a Comment