Afisa Mkuu wa Madini na Uchumi wa Bluu katika Kaunti ya Kilifi, Rahab Karisa, ameuawa katika mazingira ya kutatanisha. Rahab alidaiwa kuuawa kwa kudungwa kisu na msaidizi wake wa nyumbani eneo la Mnarani, Kaunti ya Kilifi Alhamisi asubuhi. Alirejea nchini Jumatano kutoka kwa safari ya kwenda Italia. Kulingana na mlinzi wa kibinafsi, msaidizi wa nyumba alitoroka kabla ya maafisa kutoka kampuni ya kibinafsi kufika kwa majukumu yao ya asubuhi. Kamanda wa polisi kaunti ya Kilifi Fatuma Hadi alithibitisha kisa hicho. Alisema polisi wanachunguza mauaji hayo. "Hatujui nia lakini tutajua. Tupo eneo la tukio,” alisema. Kulingana na mlinzi wa nyumba ya Karisa iliyoko eneo la Mnarani, afisa huyo wa serikali ya kaunti aliuawa kwa kudungwa kisu na msaidizi wa nyumba yake kabla ya kutoroka. Hadi alisema mwili huo uliokutwa sakafuni ulikuwa na majeraha ya kuchomwa kisu. Mwili wa marehemu umehamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Kilifi ukisubiri kufanyiwa uchung...